Vipimo
Passion fruit - 10
Karoti - 7
Ndimu - 4 kamua maji
Maji - kiasi
Sukari - kiasi upendavyo
Namna Ya Kutayarisha
- Chemsha karoti hadi ziive kisha zisage na maji katika blender.
- Kata passion fruit toa nyama weka katika mashine usage na maji
- Kisha changanya vyote katika bakulia kubwa kisha tia sukari, kisha tia ndimu
- Weka katika friji ikiwa tayari.