Jinsi ya Kutengeneza Juisi Ya Nanasi Na Tango

Vipimo
Nanasi  -  6 slesi
Tango -  1 la kiasi
Sukari -   ½ Kikombe
Barafu -  Kiasi

Namna Ya Kutayarisha
  1. Katakata nanasi na tango vipande vipande.
  2. Kisha tia kwenye mashine ya kusagia pamoja na sukari na vipande vya barafu.
  3. Ikiwa nzito sana ongeza maji.
  4. Mimina katika gilasi  
Kidokezo
Vipimo hivi ni kupata takriban gilasi 6.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.