Vipimo
Maziwa - 6 Vikombe
Sukari - ½ Kikombe
Embe iliyochujwa nzito - 1 Kikombe
Namna Ya Kutayarisha
- Changanya maziwa, sukari na urojo mzito wa embe kwenye blenda pamoja na vipande vya barafu mpaka litowe povu.
- Mimina kwenye jagi tayari kunywewa.
- Ukipenda unaweza kutia tone moja la essence ya rose.
Kidokezo:
Ukipenda unaweza kutumia rojo la embe zito lilokuwa tayari kwenye makopo (Mango Pulp)