Jinsi ya Kupika Mchuzi Wa Samaki Wa Nazi

Vipimo:


Samaki Wa Vipande                                 - 4   Vikubwa

Kitunguu maji kikubwa                            1

Tungule/nyanya                                      2

Tui zito la nazi                                        2 vikombe

Bizari ya manjano kijiko cha chai             ¼ kijiko cha chai

Pilipili mbuzi                                            3

Chumvi                                                 kiasi




Vipimo Vya Samaki Na Namna Ya Kumtayarisha Na Kumpika



Pilipii mbichi  ilosagwa                                   2 vijiko vya supu

Kitunguu saumu(thomu/galic) ilosagwa         1 kijiko cha chai

Tangawizi ilosagwa                                       1 kijiko cha chai

Mdalasini wa unga                                        ¼ kijiko cha chai

Bizari ya pilau ya unga                                  ½ kijiko cha chai

Ndimu (kamua)                                            2 

Chumvi                                                       kiasi




  1. Tia viungo vyote  katika bakuli uchanganye..

  1. Changanya na vipande vya samaki uroweke kwa muda nusu saa takriban.

  1. Mchome (grill) kwenye moto wa kiasi hadi abadilike rangi asikauke.

  1. Epua weka kando.




 Namna Ya Kutayarisha Na Kupika Mchuzi




  1. Ponda kitunguu maji na tungule (nyanya) pamoja na pilipili mbuzi moja.

  1. Tia katika sufuria pamoja na tui, weka katika moto mdogo mdogo, uache uchemke hadi tui liwe  zitozito,

  1. Mtie samaki na huku unalikoroga ili achanganyike samaki na tui.

  1. Ukipenda unaweza kutia kaa la moto ndani ya mchuzi ili kuleta ladha zaidi.


  1. Tupia pilipili mbuzi  zilobakia, ukiwa tayari kuliwa na ugali, chapati, wali au upendavyo.


Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.