Biskuti Za Mayai
Vipimo
Unga 3 Vikombe
Sukari ya unga (icing sugar) 1 Kikombe
Siagi 250 gm
Mayai 3
Vanilla 2 Vijiko vya chai
Baking powder 1 Kijiko cha chai
Namna Ya Kutayarisha Na Kupika
- Koroga siagi na sukari katika mashine ya keki (cake mixer) mpaka iwe laini (creamy).
- Tia mayai na vanilla koroga mpaka mchanganyiko uwe laini.
- Tia unga na baking powder changanya na mwiko.
- Tengeneza round upange kwenye tray utie nukta ya rangi.
- Nyunyuzia sukari juu ya hizo round ulizotengeneza kabla huja choma.
- Pika (bake) katika oven moto wa 350°F kama muda wa dakika 15 hivi huku
- unazitazama tazama.
Bis-swihhah wal-hanaa (kula kwa siha na kufurahika)