Jinsi ya kutengeneza Saladi Ya Viazi (Aina 1)

Vipimo
Viazi (mbatata) - ¼ kilo (kiasi viazi 5)   au vitano
Limau au ndimu au siki - ½ kikombe
Vitunguu nyasi   (spring onions) - 4-5 miche
Mafuta ya zaituni (oliven oil) - ½ kikombe
Chumvi - Kijiko cha chai kimoja na nusu
Namna Ya Kutayarisha Na Kupika
  1. Chemsha viazi na  maganda yake hadi viive bila ya kuvurujika
  2. Viache vipowe kisha chambua viazi ukatekate slesi au vidogodogo, mimina ndani ya bakuli kubwa.
  3. Katakata vitunguu tia kwenye viazi, tia chumvi na mafuta ya zaituni, limau  kisha vichanganye uzuri.
  4. Onja chumvi na limau ukiona yametokeza ladha basi saladi tayari kwa kuliwa.
Kidokezo:
  1. Hii ni saladi huliwa sana wakati wa majira ya joto  (summer). Waweza kula saladi hii kwa nyama ya kuchoma au samaki.
  2. Unaweza kuhifadhi kwenye friji  kwa matumizi ya siku ya pili.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.