VIPIMO
Sosi Ya tuna
Tuna (samaki/jodari) - 2 Vikopo
Vitunguu (kata kata) - 4
Nyanya zilizosagwa - 5
Nyanya kopo - 3 Vijiko vya supu
Viazi (vilivyokatwa vipande vidogo - cubes) - 4
Dengu (chick peas) - 1 kikombe
Kitunguu saumu(thomu/galic)&Tangawizi iliyosagwa 1 Kijiko cha supu
Hiliki - 1/4 kijiko cha chai
Mchanganyiko wa bizari - 1 kijiko cha supu
Chumvi - kiasi
Pilipili manga - 1 Kijiko cha chai
Vipande cha Maggi (Cube) - 2
Wali:
Mchele - 3 Vikombe vikubwa (Mugs)
Mchele - 3 Vikombe vikubwa (Mugs)
Mdalasini - 2 Vijiti
Karafuu - chembe 5
Zaafarani - kiasi
*Jirsh (Komamanga kavu au zabibu kavu -raisins) - 1/2 Kikombe
NAMNA YA KUTAYARISHA NA KUPIKA
- Kosha Mchele na roweka.
- Kaanga vitunguu hadi viwe rangi ya hudhurungi (brown) chuja mafuta uweke kando.
- Kaanga viazi, epua
- Punguza mafuta, kaanga nyanya.
- Tia thomu/tangawizi, bizari zote, vipande vya Maggi, nyanya kopo, chumvi.
- Mwaga maji ya tuna iwe kavu, changanyisha kwenye sosi.
- Tia zaafarani kidogo katika sosi na bakisha ya wali.
- Chemsha mchele pamoja na mdalasini na karafuu.
- Karibu na kuwiva, chuja maji utie katika chombo cha kupikia katika jiko (oven)
- Nyunyizia zaafarani, mwagia vitunguu, viazi, na dengu juu ya wali.
- Mwagia sosi ya tuna na pambia jirshi (au zabibu).
- Funika wali na upike katika jiko moto wa 450º kwa muda wa kupikika wali. Epua upakue.
* Jirsh ni komamanga kavu. Zioshwe vizuri kutoa vumbi au tumia zabibu kavu (raisins)