Vipimo
Siagi - Kikombe 1
Sukari - Kikombe 1
Unga - Vikombe 2
Maziwa - 1/2 (nusu) Kikombe
Mayai - 4
Baking Powder - 1 Kijiko cha supu
Arki rose - kidogo
Namna Ya Kutayarisha Na Kupika
- Washa oveni 350 - 400 Deg C liache lishike moto huku ukitayarisha mchanganyiko wa keki.
- Changanya sukari na siagi mpaka ichanganyike.
- Mimina mayai na maziwa uchanganye vizuri.
- Mimina Baking Powder kwenye unga na uchanganye vitu vyote pamoja na arki rose.
- Endelea kuchanganya vizuri mpaka uhakikishe vimechanganyika vizuri (unaweza kufanya bila ya mashine)
- Chukua trey ambayo haitojaa ukiimimina, ipake siagi na umimine mchanganyiko wako. Treya isiwe nzito sana au nyepesi sana bali iwe wastani.
- Ipike (Bake ) mpaka iwive.
- Epua iache ipoe ndio ukate kate vipande.